1.0 CHETI CHA AWALI (BASIC TECHNICIAN CERTIFICATE):
I. Mwombaji awe amefaulu angalau masomo 4 kwa kiwango cha alama “D” au zaidi kwenye mtihani wa kidato cha nne; Au
II. Awe na NVA II na ufaulu wa angalau masomo mawili kwenye mtihani wa kidato cha nne.
2.0 STASHADA (DIPLOMA):
- Aliyehitimu Cheti cha Awali (NTA Level 4) mwenye ufaulu wa masomo angalau 4 kwenye mtihani wa kidato cha nne; Au
- Aliyehitimu Kidato cha Sita mwenye ufaulu wa kuanzia Principal moja na Subsidiary moja; Au
- Aliyehitimu NVA III mwenye ufaulu wa masomo mawili kwenye mtihani wa kidato cha nne.
3.0 SHAHADA (BACHELOR DEGREE):
I. AliyehitimuKidato cha SitamwenyePrincipal passes 2 au zaidi (isipokuwamasomoyadini) najumlayaalamazisizopungua 4.0 kwatafsiriifuatayo: –
A – 5, B+ – 4, B – 3, C – 2, D – 1 (waliomalizamwaka 2014 na 2015)
A – 5, B – 4, C – 3, D – 2, E – 1 (waliomalizakablayamwaka 2014, na 2016)
Pia mwombaji awe amefauluHisabatinaKingerezakatikamtihaniwakidato cha nnekwawaombajiwaKozizaUhasibu (BAC), UnunuzinaUgavi (BPLM), naUhasibuwaFedhazaUmma (BPSAF); Au
II. AliyehitimuStashahada/NTA Level 6 mwenye GPA ya 3.5 au upper second class; Au
III. Aliyehitimu FTC mwenyewastaniwaalama “B”; Au IV. AliyehitimuStashahadayaUalimumwenyewastaniwaalama “B+”.
4.0 STASHAHADA YA UZAMILI (POSTGRADUATE DIPLOMA):
- Mwombaji awe na shahada ya kwanza au Stashahada ya Juu katika fani husika kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na NACTE/ TCU; Au
- Waliopitia kwenye bodi za fani husika (NBAA/PSPTB); Intermidiate stage au zaidi kwa NBAA na Proffesional level 3 au zaidi kwa PSPTB.