Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Abdallah Mwaipaya amewapongeza TIA kwa kutoa huduma nzuri sana kwa wateja wanaofika kwenye maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kasikazini yanayoendelea katika Viwanja vya Themi, Njiro Arusha.
“TIA ni Taasisi ambayo nimekuwa nikiisikia sana kwa elimu yenye ufanisi mnayoitoa, na leo nimethibitisha kwanini, baada ya kunipokea vizuri sana na kunielezea kuhusu  taasisi yenu ikiwa ni ushiriki wa mara ya kwanza katika Kanda hii ya Kaskazini,”. alisema DC Mwaipaya
DC Mwaipaya amesema ni muhimu TIA kama Taasisi inayotoa mafunzo, tafiti na ushauri kushiriki maonesho haya ili kutoa ushauri wa kibiashara kwa wakulima, kwa maendeleo ya mkulima mmoja mmoja lakini pia kwa Taifa kwa ujumla, kwani kauli mbiu ya mwaka huu inasema Agenda 10/30: Kilimo ni Biashara, Shiriki Kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.