Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Prof. William A. Pallangyo amefanya ziara ya kikazi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) na kukutana na Komandanti wa Chuo hicho Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Afande Lazaro Benedict Mambosasa pamoja na Afisa Mnadhimu Kamishna Msaidizi wa Polisi O.J Nselu na Mkufunzi Mkuu Kamishna Msaidizi wa Polisi L.K. Mwakyusa.
Ziara hiyo yenye  lengo la kujenga mahusiano ya kikazi baina ya TIA na DPA ambayo yataboresha taaluma kwa taaisisi zote mbili, Profesa Pallangyo amesema imekuwa fursa njema ya kukifahamu Chuo hicho na amepongeza mafanikio yaliyofikiwa na Taasisi hiyo.
Naye Afande Mambosasa ameishukuru TIA kwa kuthamini uwepo wa DPA katika  eneo jirani na Taasisi ya Uhasibu, ambapo ujio wa TIA ni kuendelea kujenga mauhusiano zaidi ya kikazi.
Katika ziara yake, Prof. Pallangyo aliambatana na Makamu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala Dkt. Issaya Hassanali, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano Bi Lillian Mpanju Rugaitika, Kaimu Meneja Mipango na Bajeti ndugu Oyombe Simba na Afisa TEHEMA Mwandamizi ndugu John Makange.
TIA ni Chuo kilichobobea kutoa mafunzo katika maeneo ya Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa Biashara, Uongozi wa Rasilimali Watu, Masoko na Uhusiano wa Umma, Uhasibu wa Umma na Fedha, Usimamizi wa Miradi, na katika nyanja nyingine za kibiashara kwa ngazi ya Cheti, Diploma, Shahada, Stashahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamili, sambamba na huduma za Utafiti na Ushauri wa Kitaalam kwenye maeneo hayo na itaendelea kuzingatia Ufanisi katika utekelezeji wa majukumu yake.
Sensa ya Watu na Makazi- Jiandae Kuhesabiwa.
Pichani ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania, Prof. William A. Palangyo akizungumza na Komandanti wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Lazaro Benedict Mambosasa
alipotembelea Chuo hicho Julai 6, 2022
Â
Pichani ni Komandanti wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Lazaro Benedict Mambosasa akizungumza na ujumbe uliongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania, Prof. William A. Palangyo, wakati wa ziara ya Prof. Palangyo DPA, Julai 6, 2022.Wa kwanza kushoto ni Dr. Isaya Hassanali, Makamu Muu wa Chuo anayeshughulikia Mipango na Utawala, wa kwanza kushoto ni Mkufunzi Mkuu Kamishna Msaidizi wa Polisi L.K. Mwakyusa
Pichani ni Komandanti wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Lazaro Benedict Mambosasa akifuatilia maoni ya Afisa Mnadhimu Kamishna Msaidizi wa Polisi O.J Nselu wa DPA wakati wa ziara ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania, Prof. William A. Palangyo, Julai 6, 2022. Wa kwanza kulia ni Dr. Isaya Hassanali, Makamu Muu wa Chuo anayeshughulikia Mipango na Utawala, wa kwanza kushoto ni Mkufunzi Mkuu Kamishna Msaidizi wa Polisi L.K. MwakyusaAfisa
A
B
Picha A na B hapo juu ni Komandanti wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Lazaro Benedict Mambosasa akifuatilia maoni ya Dr. Isaya Hassanali, Makamu Muu wa Chuo anayeshughulikia Mipango na Utawala, wa kwanzakulia, wakati wa ziara ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania, Prof. William A. Palangyo, Julai 6, 2022.
Pichani ni Komandanti wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Lazaro Benedict Mambosasa akifuatilia akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania, Prof. William A. Palangyo, alipomtembelea na kufanya mazungumzo ofisini kwake Julai 6, 2022, wa kwanza kushoto ni
Afisa Mnadhimu Kamishna Msaidizi wa Polisi O.J Nselu wa DPA na wa mwisho kushoto ni Mkufunzi Mkuu Kamishna Msaidizi wa Polisi L.K. MwakyusaAfisa
Pichani ni Komandanti wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Lazaro Benedict Mambosasa akiwa kwenye Picha ya pamoja na ujumbe uliongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania, Prof. William A. Palangyo, wakati wa ziara ya Prof. Palangyo DPA Julai 6, 2022. Wa kwanza kushoto ni
Afisa Mnadhimu Kamishna Msaidizi wa Polisi O.J Nselu, wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano kwa Umma wa TIA Bibi Lilian M. Rugaitika, wa tatu kushoto ni Meneja wa Mipango ndugu Oyombe Simba na wa kwanza kulia ni Kamishna Msaidizi wa Polisi L.K. MwakyusaAfisa na wa pili kulia ni Dr. Isaya Hassanali, Makamu mkuu wa TIA anayeshughulikia Mipango na Utawala