AFISA MTENDAJI MKUU PROF. WILLIAM AMOS PALLANGYO AANZA KAZI RASMI

April 25, 2022
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Prof. William Amos Pallangyo ameripoti leo rasmi tarehe 25/04/2022 katika Makao Makuu ya Taasisi kurasini, Dar es Salaam.
Akizungumza na Menejimenti na baadhi ya Wafanyakazi wa Taasisi, Prof. Pallangyo ameshukuru kwa mapokezi mazuri ambayo   ni ishara ya uwepo wa ushirikiano miongoni mwetu.
Aidha, amesisitiza juu ya umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja ( team work)
“Nina imani  tutafanya kazi wote kama “team”, kila mmoja ana mchango wake kulingana na dira yetu na utachangia vilivyo katika eneo ambalo umekasimiwa kufanya kazi,”. Amesema Prof. Pallangyo
Pia amesema  maadili yetu ya msingi (Core Values) ambayo ni Ubora, Ushirikiano katika utendaji kazi, Ubunifu, Weledi na Uwazi kwa pamoja yana maana kubwa  kwenye ujenzi wa Taasisi yetu, hivyo ni lazima tuyafanyie kazi kwa ufanisi wake.
Prof.Pallangyo amemaliza kwa kusema kuwa amejipanga kutembelea kila idara na kampasi kufahamu majukumu  kwa undani na namna kazi zinavyotekelezwa.
“Leo hii naanza kazi rasmi,”. Amesema Prof. Pallangyo
TIA – “Elimu kwa Ufanisi”
Kazi iendelee
/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/