TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

BAOBAB SEC SCHOOL YATEMBELEA TIA

September 26, 2022
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Dar es Salaam leo imetembelewa na Wanafunzi wa kidato cha sita 61 Wasichana 42 na Wavulana 19 mchepuo wa ECA kutoka shule ya sekondari BAOBAB, wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Stephen Mahundi  Mwalimu wa somo la Uhasibu na Mkuu wa idara ya masomo ya Biasharaamesema lengo la ziara ilikuwa kujifunza  kwa vitendo kuhusu masuala ya Uhasibu na Ukaguzi
“Wanafunzi wetu  wanatamani kuwa Wahasibu na wengine Wakaguzi tukasema tuje Taasisi ya Uhasibu Tanzania kwani ni wabobezi na mahiri wa masomo ya Uhasibu ni Chuo kikubwa na kinajulikana kwa umahiri wa masuala ya Uhasibu,”. Alisema Mwalimu Mahundi
Makamu Mkuu  Taaluma, Tafiti na Ushauri Dkt. Momole Kasambala amesema amefurahishwa sana na ujio wa wanafunzi hao katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania kujifunza kwa vitendo kuhusu masuala ya Uhasibu na Ukaguzi wa Mahesabu.
Akiongea na Wanafunzi hao Dkt. Kasambala amewaasa kuzingatia masomo yao kwa kuwa wao ni wanachuo watarajiwa
“Natarajia kuwaona wana ECA wa leo mwakani wakijiunga na TIA katika kozi za Uhasibu ili kutimiza ndoto zao za kuwa Wahasibu na Wakaguzi, nimefurahi kuwaona na kujua mnaifahamu sana Taasisi yetu, nawatakia kila la kheri katika kutimiza ndoto zenu,”. Alisema Dkt. Kasambala
Mmoja wa Wanafunzi hao wa kidato cha Sita Mchepuo wa ECA Faidha Hamisi amesema  anatamani kuwa Mhasibu na amekisikia  Chuo cha Uhasibu Kurasini, amefurahi kufika Chuo hapo na sasa amepata nguvu ya kwenda kusoma kwa bidii ili afaulu vizuri na kutimiza ndoto zake na TIA.
Dkt. Momole Kasmbala, Makam Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania, anayeshughulikia Taaluma wa akiwakaribisha na kuitambulisha Taasisi ya Uhasibu Tanzania kwa wanfunzi wa kidato cha sita wanachukua Mchepuo wa ECA Shule ya Sekondari Baobab, walipotembelea TIA leo September 23, 2022.
Mwalimu S.Mahundi wa shule ya Sekondari Baobab akiitambulisha shule ya Baobab, wanafunzi na wafanyakazi waliotembelea Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) leo Septemba 23, 2022.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Baobab wakifuatilia mada ya iliyohusu mchango wa uhasibu kwa maendeleo ya uchumi wa Tanzania, iliyowasilishwa na Mwalim Peter Mshana wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania – TIA Septemba 23, 2022.
A
B
Picha A-B hapo juu, ni baadhi ya wanafunzi wanafunzi wa shule ya Sekondari Baobab waliojibu maswali ya watoa mada kwa ufasaha, wakipokea zawadi kutoka kwa Makam Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) leo Septemba 23, 2022
/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/