TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

WIZARA YA ELIMU NA TIA YASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO

December 3, 2022
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt. Francis Michael na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania ( TIA) leo tarehe 1,Disemba 2022 wamesaini Mkataba wa Makubaliano baina ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia chini  ya mradi wa “Higher Education for Economic Transformation”( HEET) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Francis Michael  amesema mradi umelenga kujenga na kukarabati Vyumba vya mihadhara na madarasa 130, hosteli 34, Maabara na karakana 108, vyumba vya Semina 55, vyumba vya mikutano ya kisayansi 23 na miundombimu ya mashambani  10 na kuwajengea uwezo wahadhiri katika Taasisi za Elimu ya Juu kwa kuwasomesha wahadhiri zaidi ya 831 katika ngazi ya shahada ya Uzamivu na Umahiri.
Aidha, Dkt. Michael aliongeza kuwa mradi huu utahusisha na kuandaa zaidi ya mitaala 290 katika fani za Kipaumbele ili iendane na mahitaji ya soko la ajira  ndani na nje ya nchi
na kuimarisha miundombinu na matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji, na kuboresha mifumo ya uendeshaji wa Taasisi za Elimu ya Juu.
Afisa Mtendaji Mkuu Profesa Pallangyo ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha na kuongeza miundombinu ya kufundishia na kujisomea katika Kampasi ya Singida ikiwa ni lengo la kuhakikisha Vyuo vikuu vinakuwa hadi pembezoni mwa nchi ya Tanzania.
Utiaji saini huu umehusisha Vyuo vikuu vilivyopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, na kuhudhuriwa na waratibu wakuu na wasaidizi kutoka katika taasisi hizo akiwemo Bi. Halima Muhkisin Afisa Ugavi na Manunuzi TIA.
Utekelezaji wa mradi wa HEET utaongeza udahili katika fani za kipaumbele cha Taifa kutoka 40,000 mwaka 2020 hadi kufikia 100,600 mwaka 2026.
/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/