Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Prof. William Pallangyo amepokea Wimbo wa Taasisi kutoka kwa watunzi walioibuka washindi katika kinyangangiro cha kutafuta wimbo bora wa TIA.
Katika hafla fupi ya makabidhiano ya wimbo huo Profesa William Pallangyo amewashukuru na kuwapongeza wote walioshiriki shindano hilo na kuonesha uwezo mkubwa wa utungaji,
“Sikuzote kwenye mashindano lazima apatikane mshindi mmoja, nawapongeza  mshindi wa kwanza Kwani haikuwa rahisi katika uchambuzi wa Wimbo  pia na kuweza  kufanya  Wimbo  huo kuwa na maudhui  mazuri ambao unaenda kuishi katika kizazi cha TIA miaka mingi,”. Alisema Profesa Pallangyo
Aidha Profesa Pallangyo amekabidhi zawadi kwa washindi wa 3 walioibuka kidedea ikiwa mshindi wa kwanza ambaye ni Mt. Frasisko wa Assisi amepata Cheki ya fedha taslimu Millioni 2, wa pili Gwanko Amani Ezra Milioni 1Â Â kutoka Dar es Salaam na TIA Kigoma wakiwa washindi wa 3 na kupata Laki tano
Pia Profesa Pallangyo ametoa tamko rasmi la utumiaji wa Wimbo huo  katika  shughuli zote na matukio yote ya Taasisi  ya Uhasibu Tanzania kwa Kampasi zake zote Nchini.
Naye  Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Dkt. Momole Kasambala amewapongeza washiriki wote walio shiriki katika utungaji wa Wimbo na kumpongeza mshindi wa Kwanza kwa maudhui bora yaliyomo katika wimbo huo.
Hafla hiyo iliambatana na utiaji wa saini wa mkataba wa haki miliki wa Wimbo  kati ya Mkuu wa Chuo Profesa William Pallangyo  na Mt. Frasisko wa Assisi ( mshindi wa kwanza )  na kushuhudiwa na Mwanasheria Bi. Penila Muganda, Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Dkt Momole Kasambala, Mkurugenzi  Wa Rasilimali Watu Bw. Thomas Mabeba , Kamati ya mchakato wa Wimbo huo, Serikali ya Wanafunzi (TIASO), Mshindi wa pili na watatu pamoja na wageni waalikwa.