Mkataba wa ujenzi wa majengo ya Kampasi ya Kigoma umesainiwa baina ya TIA na Kampuni ya Masasi Construction ulofanyika mapema wiki hii, 2023 Â mkoani Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Prof. William Pallangyo akiongea katika hafla hio ya utiaji saini wa mkataba wa mradi huo, amemtaka mkandarasi kukamilisha ujenzi huo kwa viwango na wakati uliopangwa pamoja na kuzingatia thamani ya fedha ya mradi (Value for Money) wakati wa ujenzi na kuhakikisha wanakabidhi mradi kwa muda uliopangwa.
Prof Pallangyo ameongeza kuwa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kampasi ya Kigoma ni mkakati wa serikali kuboresha miundombinu huku fedha za utekelezaji wa mradi huo zikitoka serikalini kwa asilimia mia moja na ni miongoni mwa miradi muhimu kitaifa na kimataifa kwani tunategemea wanafunzi kutoka mikoa jirani na nchi jirani kama DRC,Burundi  na Rwanda”alisema
“Natoa wito kwa mkandarasi wa mradi huu kampuni ya Masasi Construction LTD kufanya kazi yake kwa weledi wa hali ya juu ili kazi zote zikamilike ndani ya muda uliopangwa na kwa viwango na gharama zilizokubalika” alisisitiza Prof Pallangyo.
Naye Rimit Ladwa ameishukuru TIA na ameahidi  kuwa Masasi Construction Ltd itatekeleza mradi huo muda uliopangwa. Mkataba huu wa mradi  wa ujenzi umeshuhudiwa na Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Fedha na Utawala Dkt. Issaya Hassanali,Mkurugenzi wa Fedha na Uhasibu Bukard Haule,Mkurugenzi wa Huduma za wanafunzi Luciana Comino na wajumbe wa kamati.





