Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Dar es salaam leo tarehe 16/03/2023 imetembelewa na wanafunzi wapatao 62 wasichana wa kidato cha III na V mchepuo wa ECA, shule ya sekondari BaoBab wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Ziara hiyo imeongozwa na Mwalimu Stephen Mahundi, ambaye amesema lengo kuu la ziara ya wanafunzi hao ni kujifunza kwa vitendo kwenye mambo ya Uhasibu na Ukaguzi kutokana na mchepuo wanaosomea, pia mafunzo pia ziara hii itawawezesha wanafunzi kufanya maamuzi sahihi wakati wa kuchagua kozi sahihi mara watakapohitimu masomo yao ya Sekondari.
kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma (Ag.DR-ARC) Amosi Manyama, ambaye aliwakaribisha na kuwaeleza kwa ufupi kozi zinazotolewa, Aidha amewataka kuzingatia masomo yao.
Naye kaimu mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho (Ag.HRCP) Dkt Maiga. Alisema amefurahishwa sana na ujio wa wanafunzi hao na kuwapongeza wanafunzi wa 3 wenye ufaulu wa daraja la kwanza kwenye matokeo yao ya kidato cha nne kuingia kidato cha tano, pia amewapongeza wanafunzi walioweza kujibu maswali kwa ufasaha yaliyoulizwa wakati wa mafunzo hayo.
Wanafunzi wetu wanatamani kuwa wahasibu na wengine wakaguzi na wamevutiwa kuja kujifunza zaidi kwa vitendo chuoni hapo. Amesema Mwalimu Mahundi aliendelea kusema TIA mmekuwa na mchango mkubwa sana kwa Wanafunzi wa mchepuo wa Biashara kwa kuwapatia muongoza sahihi uongozi wa Baobab unawashukuru sana.
Naye CPA Mutaju Marobhe miongoni mwa watoa mafunzo aliweza kuwaelezea wanafunzi hao juu ya uhusiano wa wanafunzi wa mchepuo wa ECA na utendaji wa taaluma ya Uhasibu, na kuwaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao. Pia anatarajia kuwaona wanafunzi hao wakijiunga na TIA.
Nancy Pallangyo mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari Baobab aliweza kuishukuru TIA kwa kuwapatia mafunzo ambayo yatawafanya wawe na maamuzi sahihi wakati wa kuchagua kozi wanazotaka wafikapo ngazi ya elimu ya juu.