TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

UJENZI WA KAMPASI YA TIA KIGOMA KUANZA MACHI 

January 26, 2023
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe. Esther Mahawe ametembelea eneo la Taasisi ya Uhasibu Tanzania lililopo Kamala, Manispaa ya Kigoma ambapo ujenzi wa Kampasi ya Kigoma unatarajia kuanza mapema Machi 2023.
Katika ziara hiyo Mhe.Mahawe ameipongeza TIA kwa kuanzisha ujenzi wa Kampasi ya kisasa katika ukanda wa magharibi ambapo itakuwa ni fursa kubwa kwa wananchi  kwani kitakuwa  Chuo cha Kitofauti katika Manispaa ya Kigoma na Mkoa mzima kwa ujumla.
Aidha, Afisa Mtendaji Mkuu Profesa Wiliam Pallangyo amesema ujenzi wa awamu ya kwanza unatarajiwa kukamilika mwezi disemba 2024 ambao utahusisha ujenzi wa Jengo la Utawala lenye Ofisi 21, Maktaba yenye uwezo wa kuhudumia Wanachuo 250 kwa wakati mmoja, Maabara ya Kompyuta y kisasa yenye uwezo wa kuhudumia Wanachuo 200, Kafteria yenye uwezo wa kuhudumia Wanachuo 180.
Pia Profesa Pallangyo amesema ujenzi wa mradi huu utagharimu kiasi cha shilingi Bil.12.5 ambazo zimetolewa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Fedha na Mipango.
Kwa pamoja Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Ukaguzi wa Bodi ya Ushauri ya Wizara, Dkt. Nicolaus Shombe (Mwenyekiti Kamati ya Fedha na Utawala), Bw. Thabiti Dokodoko (Mwenyekiti Kamati ya Ukaguzi) na Bi Mystica  Ngongi wameipongeza TIA kwa hatua kubwa iliyofikiwa katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kampasi na pia wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya kusomea na kufundishia.
Ujenzi  wa mradi huu kwa TIA Kampasi ya Kigoma umelenga kutumia majengo yao, na si kama sasa ambavyo inatumia majengo ya kukodisha kutoka ofisi za “RedCross”.
TIA – “Elimu kwa Ufanisi “
Kazi Iendelee
/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/