TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

TIA YAWAWEZESHA WANACHUO KUANDAA WAZO LA BIASHARA

November 12, 2022

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu (TIA) Profesa William Pallangyo amefungua kongamano la  mafunzo ya Ujasiriamali na ujuzi wa kitaluma kwa Wanafunzi wa TIA Kampasi ya Mbeya lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kuanzisha wazo la biashara na kulifanyia kazi.

Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa Karume ambapo amesema mpango wa Taasisi ni kuwafanya wanachuo wakihitimu mafunzo yao wawe tofauti kwa kuona fursa katika mazingira yanayowazunguka, jinsi ya kusimamia miradi watakayoanzisha kwa kujiajiri na umahiri wa kufanya usaili wakati wa kuajariwa.

“Ni vyema kuajiriwa lakini ikitokea hujapata ajira je utafanya nini?  kusoma ni jambo moja na baada ya kusoma unaenda wapi? ni jambo jingine,  leo kwenye kongamano hili utajifunza kuandaa wazo, kuliwekea mpango na kulitekeleza,”. amesema Profesa Pallangyo.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Fedha, Mipango na Utawala Dkt.Issaya Hassanal  amesema TIA imejipanga kuwaongoza na kuwaelekeza maono mbalimbali waliyonayo  katika ujasiriamali kwani wanategemewa na wazazi kwa kufurahia matunda yao na taifa pindi watakapopata kipato kitachowapelekea kulipa kodi.

Kongamano hilo limehudhuriwa na wadau mbalimbali waliofanikiwa katika sekta ya ujasiriamali akiwemo Aliko Richard Mkurugenzi Mtendaji Allly Rich Arts Ltd ambaye amewaasa vijana kuheshimu mawazo yao ya kibiashara na kuyafanyia kazi pasipo kukata tamaa, wanachuo wanaohitimu pamoja na wanaoendelea.

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/