Taasisi ya Uhasibu Tanzania imetoa mafunzo ya ununuzi na usimamizi wa mikataba kwa idara ya Ugavi na Ununuzi na Wajumbe wa tenda Bodi  16 kutoka Wakala wa Maji Vijijini ( RUWASSA) kanda ya ziwa kwa siku 4 kuanzia tarehe 12 mpaka tarehe 15, disemba 2022 katika ukumbi wa TIA Jijini Dar es Salaam.
Lengo la mafunzo hayo  ni kukumbushana juu ya masuala mbali mbali katika ununuzi wa Umma Ikiwemo sheria ya ununuzi wa Umma, taratibu za kuandaa mpango wa mwaka wa Ununuzi, taratibu ya Ununuzi kwa Zabuni,  usimamizi wa mikataba pamoja na  uuzaji wa mali za Umma  kwa Zabuni.
Mafunzo hayo yametolewa na Dkt. Hemed Msuya ambaye ni mhadhiri mbobezi katika kada ya Ununuzi na Ugavi, ambapo amesema ni muhimu Maafisa Ugavi na Ununuzi kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za ununuzi wa Umma ili kuepuka udanganyifu wowote unaoweza kujitokeza.
Dkt. Msuya amesema mafunzo haya yawe chachu kwa Maafisa Ugavi na Ununuzi kuendelea kujifunza zaidi ili kuepuka sitonfahamu zinazojitokeza wakati wa manunuzi ya vifaa vya umma katika Taasisi au mashirika ya Umma.
Mafunzo hayo yalihitimishwa kwa Washiriki kupewa Vyeti ikiwa ni uthibitisho wa kuwa wamepata mafunzo ambayo yatasaidia kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
TIA inaendelea kutoa mafunzo kwa taasisi mbali mbali za Umma ili kuboresha utendaji kazi katika ofisi za Umma

