TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

TIA YASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO NA MS TCDC

May 10, 2023
Leo tarehe 08/05/2023, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Prof. William Pallangyo na Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa “MS Training Centre for Development Cooperation” Dkt. Makena Muthuri wamesaini mkataba wa makubaliano kwa lengo la kushirikiana katika maeneo mbalimbali.
Mashirikiano hayo yamejikita  katika kuandika mapendekezo ya kupata fedha (Grant Proposals) kutoka kwa Serikali au sekta ya umma, kuendesha  kozi za muda fupi (Short Courses) ndani ya TIA na TCDC,  ufuatiliaji wa tathmini ya uwajibikaji na ujifunzaji uongozi wa mageuzi.
Afisa Mtendaji Mkuu Profesa Pallangyo pia aliongeza kuwa mashirikiano hayo yanalenga kuimarisha uwezo wa wafanyakazi ( Capacity building for staff) wa TCDC na TIA, kufanya mafunzo ya Kiswahili huko Zanzibar wakati TIA inapata wanafunzi na kuunda kongamano ili kujibu wito wa mashauriano na mapendekezo kutoka USAID na taasisi nyingine za ufadhili wa kimataifa.
Naye Dkt.  Makena amesema TIA na TCDC wamelenga pia kuwa na ushirikiano wa pamoja katika kufanya Shahada ya Sanaa na Mpango wa Utawala na Maendeleo, kuandaa warsha, mikutano,  machapisho  ya pamoja katika majarida yanayopitiwa na wenzao, ikiwemo “Web of Science” na “database ya Scopus”
“Kupitia Taasisi hizi mbili kutawezesha  programu ya maandalizi ya kitaaluma kwa wanafunzi kuhusiana na ujuzi wa karne ya 21,”. Alisema  Dkt.Makena
Mkataba huu wa makubaliano umeshuhudia na wanasheria wa TIA Saidi Mayunga na MS TCDC Bi. Doris Likwelile, Mkuu wa Taaluma Dkt. Irene Lugalla, Mkuu wa sehemu ya Utafiti na Mahusiano ya Nje Dkt. Yohana Maiga, na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na Masoko Bi. Lilian Rugaitika.
Kazi Inaendelea
/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/