TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

TIA YASAINI  MKATABA  WA MAKUBALIANO NA GLOBAL EDUCATION LINK

April 24, 2023

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Education Link  Bw.Abdumalik S. Mollel  wamesaini mkataba wa makubaliano baina ya Global Education Link ambao ni Wakala wa vyuo  Vikuu vya nje ya Nchi .

Katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni wa Global Education Link  Bw. Abdumalik S. Molel amesema wameingia makubaliano hayo lengo likiwa ni  kuunganisha TIA na Vyuo Vikuu vya nje ya Nchi ili kujenga ushirikiano.

Mkurugenzi Mollel aliongeza kuwa Mkataba huu wa Makubaliano ni hatua ya kwanza ya mashirikiano ya TIA na Vyuo Vikuu vya Kimataifa ambavyo vina shirikiana na Global Education Link visivyo pungua 300 kutoka Sehemu mbalimabali duniani.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu  wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Prof.William Pallangyo ameeleza kuwa mkataba  huu utaifanya TIA kuwa chuo kitakacho jitangaza vizuri nje ya nchi na kujifunza kutoka kwa wenzetu kwenye maeneo ya Mitaala, Tafiti, Machapisho na Tekinolojia.

“Pia ni nafasi kwa TIA   kuwapa  fursa Wanachuo  ya kuweza kujifunza  kutoka kwa vyuo tutakavyo shirikiana navyo, hata hivyo  kwa ushirikiano huu wa vyuo vikuu vya nje ya nchi na TIA kupitia Global Education Link, tunategemea wahadhiri wetu kuweza kunufaika na Mafunzo ya juu yaani PhD na kufanya tafiti kwa kushirikiana na wataalamu wa nje ya nchi,.” Alisema Profesa Pallangyo

Mkataba huu wa Makubaliano umeshuhudiwa na Wanasheria wa TIA na Global Education Link, Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Dkt. Momole Kasambala , Mkurugenzi wa Taaluma Dkt. Mugisha Kamala , Mkurugenzi wa Huduma Mtambuka za Taaluma Dkt. Modest Asenga, Mkurugenzi wa huduma za Maktaba Dkt.Bahati Shagama, na Mkuu wa sehemu ya Machapisho na Mauhusiano ya nje Dkt.Yohana Maige

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/