TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

TIA YASAINI MAKUBALIANO YA MASHIRIKIANO NA KAMPUNI ZA SPEKI TECHNOLOGIES NA SOMAPP FOUNDATION

January 31, 2023

Leo Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Prof. William A. Pallangyo wamesaini Makubaliano ya Mashirikiano na Isaya Yunge Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni mbili za SPEKI Technologies na SOMAPP Foundation za Jijini Dar es Salaam.

Mashirikiano yataleta ubunifu na kuongeza tija na ufanisi wa matumizi ya TEHAMA kwa Watumishi na Wanachuo wa TIA.

Aidha, utekelezaji wa mashirikiano hayo, utawaandaa wanachuo kujitegemea na kukuza ujuzi wa kujiajiri na kutengeneza ajira ili kuendana na kauli mbiu ya TIA – “Elimu kwa Ufanisi”.

Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Wanasheria wa TIA na SPEK, Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Taaluma Dkt.Momole Kasambala, Mkuu wa Idara ya Tafiti na Ushauri Dkt.Abdallah Gorah na Imani Matonya Mratibu wa Maendeleo ya Kitaaluma TIA.

 

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/