Taasisi ya Uhasibu Tanzania kwa kushirikiana na asasi ya madini plus  pamoja na TBC Taifa redio wameendesha mdahalo juu ya nidhamu ya fedha katika vyanzo mbalimbali ikiwemo Mikopo ya Chuo, Ujasiliamali pamoja na wanaowezeshwa na wazazi kwa wanachuo takribani 20 katika ukumbi wa TIA Dar es salaam.
Mdahalo huo umelenga kuwasaidia wanachuo hao kuwa na  matumizi  sahihi ya pesa kwa utunzaji  wa fedha katika uwekezaji wa fedha kwenye biashara ndogo ndogo, uwekaji wa akiba wa fedha  ili ziweze kumkwamua mwanachuo kimaisha na kuepukana na tamaa mbaya wakiwa chuoni.
Katika mdahalo huo, vijana wamepata nafasi ya kutoa mawazo yao, kuuliza maswali na kubadilisha uzoefu na wawezeshaji ambapo wameomba mafunzo ya namna hii yaendelee kutolewa mara kwa mara ili wanapohitimu wakawe msaada katika jamii inayowazunguka.
Upande wa wawezeshaji wa TIA waliongozwa na Ndg. Imani Stanley Matonya ambaye ni mratibu wa kitengo cha ujasiliamali, vituo atamizi na ukuzaji wa taaluma na utaalam, Peter Mshana mhadhiri mbobezi katika fani ya Uhasibu na Fedha na Stephen Mashauri ambaye ni mshauri wa Wanafunzi.
Nao upande wa Madini plus waliongozwa na Ndg. Justine Kufakuwoja Mratibu Madini Plus, Ndg. Ally Mkimo Mwenyekiti Madini Plus na mtangazaji wa kipindi cha Kona ya vijana,  Ndg Ezekiel Shamakala Mtayarishaji vipindi TBC Taifa pamoja na mhitimu wa TIA Ndg. Rashidi S. Kamagezi –  Mkurugenzi wa  Msomiflix Africa.







