Afisa Mtendaji Mkuu Prof. William Pallangyo amekata keki iliyotengenezwa na Mwanachuo mjasiriamali Mohamed Kaisi anayesoma Kampasi ya Mtwara ngazi ya Diploma, ikiwa ni ishara ya kuendeleza ubunifu wa wanachuo wa kujifunza kwa vitendo na kukuza wazo biashara la Mwanachuo.
Profesa Pallangyo amesema wazo biashara ni muendelezo wa kuwajengea uwezo wanachuo kujiajiri kupitia elimu ya darasani
“Tuna Wanachuo wabunifu katika mawazo ya biashara mbalimbali, hii ni faraja kubwa kuona vijana wana mawazo ya msingi ambayo yakiendelezwa watafika mbali,”. Amesisitiza Profesa Pallangyo
Hafla hiyo fupi ya kukata keki imehudhuriwa na Makamu Mkuu wa Chuo Fedha, Utawala na Mipango Dkt. Issaya Hassanal, Kampasi Meneja wa Mtwara Dkt. Godwin Mollel, Â Bi.Damari Tandas ambaye ni mratibu wa maendeleo ya kitaaluma na Kitaalam pamoja na Wanachuo wa TIA katika Ukumbi wa Kampasi ya Mtwara Mjimwema.
Â
/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/