Leo tarehe 07/03/2023 Wafanyakazi Wanawake wa  Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kuelekea maadhimisho ya Siku  ya Wanawake Duniani wametembelea Gereza la Segerea Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa wanawake TIA Latifa Adam amesema ni vema kujenga utaratibu wa kuwatembelea wafungwa  ambao kwa namna moja au nyingine wamejikuta wapo gerezani kwa makosa mbalimbali,  lengo kuu  la kuwatembelea ni kuwaonesha upendo, kuwafariji, kuwatia moyo  kuwa wapo mahali sahihi ili kurekebisha walipokosea.
Naye Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa TIA Witness Mbura amesema imezoeleka watu kusaidia vikundi vingine maalumu na kusahau wafungwa, hivyo wanawake wa TIA Â wamejitolea kuwasaidia mahitaji mbalimbali na muhimu wakati wakitumikia vifungo vyao.
Kwa niaba ya Mkuu wa Mageteza S.P Kasomwa ameishukuru Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kupitia umoja wa wanawake wa Taasisi hiyo kwa kujitoa kwa dhati kuwakumbuka wafungwa wanawake kwa mahitaji mbali mbali yenye umuhimu.



