Bodi ya Ushauri ya Wizara imetembelea mradi wa Ujenzi wa Jengo la Taaluma Kampasi ya Mwanza, hapo jana. Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara Wakili Said Chiguma amesema TIA imedhamiria kuboresha mazingira wezeshi ya miundombinu ya kusomea na kufundishia kwa Kampasi zake zote,
“Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan anaendelea kutekeleza kwa kiwango cha juu na kasi katika sekta ya Elimu, lengo likiwa kuhakikisha Wananchi wengi wanapata elimu ya kujiajiri na kuajiriwa,”. Alisema Wakili Chiguma
Naye Afisa Mtendaji Mkuu Profesa Pallangyo amesema Taasisi imejipanga vyema kukabiliana na ongezeko la wakazi wa Kanda ya Ziwa wanaohitaji huduma zinazotolewa na TIA katika kutoa mafunzo, ushauri wa kiuchumi na tafiti zenye kutatua changamoto kwa wakazi wa kanda ya Ziwa.
Aidha, wajumbe wa Bodi kwa ujumla wake wameipongeza Menejimenti kwa maendeleo mazuri ya ujenzi na kutoa wito wa kukamilisha mradi huo kwa wakati ikiwa ni juhudi za Serikali ya awamu ya sita.
Ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara Wakili Said Chiguma Musendo pamoja Wajumbe wengine, Katibu (Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA) Prof. William Pallangyo, Dkt. Leonada Mwagike, Bw. Thabit Dokodoko, Mystica Ngongi, na Bi. Emma Lyimo. Wakiambatana na wenyeji Mkurugenzi wa Kampasi ya Mwanza Dkt. Honest Kimario, Mratibu wa Taaluma Bw. Vicent Kwambiana na Mratibu wa Mradi Bw. Godfrey Seni.





