Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Suleimani Mwenda akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter Serukamba alisema Serikali itaendelea kutenga Fedha kuwezesha Taasisi za Elimu ya Juu kuboresha mazingira ya kujifunzia na kusomea,ikiwa ni moja ya dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Vyuo vya Elimu ya kati na juu vinatoa elimu bora inayoendana na wakati tuliopo
Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Wakili Said Musendo Chiguma ametoa wito kwa wahitimu wa Kampasi ya Singida kutumia elimu waliopata TIA kutatua changamoto zilizopo katika jamii na kusisitiza kuwa Jamii na Taifa kwa ujumla wanategemea kuona ujuzi mlioupata TIA unawapa fursa mbalimbali za kujiajiri na kutengeneza ajira kwa wengine.
Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Prof. William Pallangyo aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Taasisi kwa kutoa mikopo kwa Wanafunzi, na kusema “TIA imeendelea kutekeleza majukumu yake makuu ya kutoa mafunzo, kufanya utafiti na kutoa huduma ya ushauri wa kitaalam kwa kuongeza ufanisi.”