TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

TIA NA JESHI LA POLISI TANZANIA WAFUNGUA UKURASA MPYA KWA KUTIA SAINI HATI YA MASHIRIKIANO

September 17, 2023

Tarehe 15 Septemba 2023 Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na Jeshi la Polisi Tanzania (TPF) zimeandika historia ya mashirikiano ambayo yatatekelezwa baina ya TIA na TPF kupitia Chuo cha Taaluma ya polisi Dar es salaam yaani ‘Dar Es Salaam Police Academy (DPA), makubaliano haya, TIA na DPA watashirikiana katika masuala mbalimbali ya kitaaluma ikiwemo Kufanya tafiti , Kuendesha makongamano ya kitaaluma pamoja na kujengeana uwezo katika maeneo bainishi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA Prof. William Pallangyo alisema “hii ni hatua muhimu kuhakikisha tunaendelea kukuza wigo wa kiutendaji, kukuza mahusiano mazuri na yenye tija kwa pande zote.Pia Mashirikiano Haya yatatuwezesha kupata majawabu ya changamoto za kiuchumi na kijamii zinazolikabili Taifa na kuchagiza maendeleo ya kiuchumi, hivyo, kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Sisi Jeshi la Polisi Tanzania katika ngazi ya Makao Makuu tunayo nia ya dhati ya kuhakikisha kuwa ushirikiano huu baina yetu na TIA unatekelezwa na kuliletea Taifa letu manufaa makubwa kwa kuwa malengo yake  yanaendana na sera na mipango ya serikali ili kuweza kufikia malengo makuu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025, hususani katika kudumisha Amani, Usalama na Kujenga uchumi imara unaoweza kukabiliana na ushindani unaoendelea duniani kwa kuzingatia maendeleo ya sayansi na teknologia.”Alisema Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camillius M. Wambura.

Aidha SACP Dr. Lazaro Benedict Mambosasa Alisema “Mashirikiano haya ya pande zote mbili yamelenga katika maeneo yafuatayo; Kutoa Mafunzo mbalimbali ya kiusalama kwa watumishi na Jumuiya ya TIA kwa ujumla, Kuendesha Mafunzo ya muda mfupi na ya muda mrefu kwa Watumishi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Watumishi wa TIA, na wanafunzi wa DPA na TIA, Kushirikiana katika masuala ya kufanya tafiti timizi, ushauri wa kitaalam na uchapishaji katika maeneo mbalimbali ya kitaaluma,Kushirikiana katika Uandishi wa Maandiko ya Miradi.

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/